Zaburi114
Listen to this chapter
0:00
0:00
Mungu Awaongoza Israeli Kutoka Misri
1
Wakati Israeli walipotoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,
2
Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake.
Uumbaji Waguswa na Uwepo wa Mungu
3
Bahari ilitazama ikakimbia, Yordani ulirudi nyuma,
4
milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo.
Maswali kwa Uumbaji
5
Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,
6
enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo?
Uwepo wa BWANA Wadai Kicho
7
Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo,
8
aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.
Use ← → arrow keys to navigate
Settings
Reading Style
Typeface
Font Size px
Reading Width chars
Options
Study Note