Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Goat

8 mistari · 4 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Bwana akawaambia Mose na Aroni,

  2. “Waambieni Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote waishio juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala:

  3. Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua.

  4. “ ‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; kwa kawaida ya ibada hiyo ni najisi kwenu.

  5. Pelele ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.

  6. Sungura ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.

  7. Naye nguruwe ingawa anazo kwato zilizogawanyika sehemu mbili, hacheui; huyo ni najisi kwenu.

  8. Kamwe msile nyama yao wala kugusa mizoga yao; wao ni najisi kwenu.