Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Abihail

5 mistari · 4 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.

  2. Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.

  3. Rehoboamu alimwoa Mahalati ambaye alikuwa binti Yeremothi mwana wa Daudi, mamaye alikuwa Abihaili binti Eliabu mwana wa Yese.

  4. Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu.

  5. Zamu ya Esta ilipofika kwenda kwa mfalme (msichana ambaye Mordekai alikuwa amemlea, binti wa Abihaili mjomba wake), Esta hakutaka vitu zaidi ya vile ambavyo Hegai, towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake alivyokuwa amemshauri. Naye Esta alipata kibali kwa kila mtu aliyemwona.