Skip to content

Zabdi

4 mistari · 6 wanafamilia

Anajulikana pia kama: Zimri

Mistari inayomtaja Zabdi

  1. Lakini Waisraeli hawakuwa waaminifu kuhusu vile vitu vilivyowekwa wakfu; Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alivichukua baadhi ya hivyo vitu. Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Israeli.

  2. Koo za Yuda zikaja mbele, naye akawatwaa Wazera. Akaamuru ukoo wa Wazera kuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ya Zabdi ikatwaliwa.

  3. Yoshua akaamuru watu wa jamaa ya Zabdi kuja mbele mtu kwa mtu, naye Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, akatwaliwa.

  4. Wana wa Zera walikuwa: Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.