Zaburi 9:13-18
13
Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,
14
ili niweze kutangaza sifa zako katika malango ya Binti Sayuni na huko niushangilie wokovu wako.
15
Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.
16
Bwana anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.
17
Waovu wataishia kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
18
Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.
Settings