Skip to content
Zaburi 88:8-16

Zaburi 88:8-16

8
Umenitenga na rafiki zangu wa karibu na kunifanya chukizo kwao. Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka;
9
nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee Bwana, ninakuita kila siku, ninakunyooshea wewe mikono yangu.
10
Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?
11
Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu?
12
Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?
13
Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie; asubuhi maombi yangu huja mbele zako.
14
Ee Bwana, kwa nini unanikataa na kunificha uso wako?
15
Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.
16
Ghadhabu yako imepita juu yangu; hofu zako zimeniangamiza.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options