Zaburi 86:1-7
1
Maombi ya Daudi. Ee Bwana, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.
2
Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, wewe ni Mungu wangu, mwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
3
Ee Bwana, nihurumie mimi, kwa maana ninakuita mchana kutwa.
4
Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, ninainua nafsi yangu.
5
Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao.
6
Ee Bwana, sikia maombi yangu, sikiliza kilio changu unihurumie.
7
Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu.
Settings