Zaburi 85:8-13
8
Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: lakini nao wasirudie upumbavu.
9
Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.
10
Upendo na uaminifu hukutana pamoja, haki na amani hubusiana.
11
Uaminifu huchipua kutoka nchi, haki hutazama chini kutoka mbinguni.
12
Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema, nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.
13
Haki itatangulia mbele yake na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.
Settings