Skip to content
Zaburi 76:1-9

Zaburi 76:1-9

1
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo. Katika Yuda, Mungu anajulikana, jina lake ni kuu katika Israeli.
2
Hema lake liko Salemu, makao yake katika Sayuni.
3
Huko alivunja mishale imetametayo, ngao na panga, silaha za vita.
4
Wewe unangʼaa kwa mwanga, mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori.
5
Mashujaa hulala wametekwa nyara, hulala usingizi wao wa mwisho; hakuna hata mmoja wa watu wa vita anayeweza kuinua mikono yake.
6
Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, farasi na gari la vita vilikaa kimya.
7
Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa. Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika?
8
Kutoka mbinguni ulitamka hukumu, nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya:
9
wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, kuwaokoa wote walioonewa katika nchi.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options