1
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo. Katika Yuda, Mungu anajulikana, jina lake ni kuu katika Israeli.
2
Hema lake liko Salemu, makao yake katika Sayuni.
3
Huko alivunja mishale imetametayo, ngao na panga, silaha za vita.