Zaburi 72:7-14
7
Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.
8
Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia.
9
Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi.
10
Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi.
11
Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.
12
Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.
13
Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.
14
Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.
Settings