Zaburi 68:28-35
28
Ee Mungu, amuru uwezo wako, Ee Mungu tuonyeshe nguvu zako, kama ulivyofanya hapo awali.
29
Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu wafalme watakuletea zawadi.
30
Mkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi, kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa. Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea. Tawanya mataifa yapendayo vita.
31
Wajumbe watakuja kutoka Misri, Kushi atajisalimisha kwa Mungu.
32
Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, mwimbieni Bwana sifa,
33
mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu.
34
Tangazeni uwezo wa Mungu, ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, ambaye uwezo wake uko katika anga.
35
Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. Mungu Asifiwe!
Settings