Skip to content
Zaburi 37:17-22

Zaburi 37:17-22

17
kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, lakini Bwana humtegemeza mwenye haki.
18
Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele.
19
Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu.
20
Lakini waovu wataangamia: Adui za Bwana watakuwa kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi.
21
Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.
22
Wale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi, bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options