Zaburi 25:16-22
16
Nigeukie na unihurumie, kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka.
17
Shida za moyo wangu zimeongezeka, niokoe katika dhiki yangu.
18
Uangalie mateso na shida zangu na uniondolee dhambi zangu zote.
19
Tazama adui zangu walivyo wengi, pia uone jinsi wanavyonichukia vikali!
20
Uyalinde maisha yangu na uniokoe, usiniache niaibike, kwa maana nimekukimbilia wewe.
21
Uadilifu na uaminifu vinilinde, kwa sababu tumaini langu ni kwako.
22
Ee Mungu, wakomboe Israeli, katika shida zao zote!
Settings