Zaburi 116:3-6
3
Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni.
4
Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!”
5
Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma.
6
Bwana huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.