Rukia maudhui
Zaburi 107:23-32

Walio Hatarini Baharini: Mfano wa Nne

Zaburi 107:23-32
23
Wengine walisafiri baharini kwa meli, walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.
24
Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini.
25
Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu.
26
Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.
27
Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, ujanja wao ukafikia ukomo.
28
Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawatoa kwenye taabu yao.
29
Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, mawimbi ya bahari yakatulia.
30
Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.
31
Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.
32
Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options