Mithali 31:1-9
1
Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:
2
“Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu, ee mwana wa nadhiri zangu,
3
Usitumie nguvu zako kwa wanawake, uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.
4
“Ee Lemueli, haifai wafalme, haifai wafalme kunywa mvinyo, haifai watawala kutamani sana kileo,
5
wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa.
6
Wape kileo wale wanaoangamia, mvinyo wale walio na uchungu,
7
Wanywe na kusahau umaskini wao na wasikumbuke taabu yao tena.
8
“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea, kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.
9
Sema na uamue kwa haki, tetea haki za maskini na wahitaji.”
Settings