Mithali 29:19-27
19
Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu, ajapoelewa, hataitikia.
20
Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.
21
Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, atamletea sikitiko mwishoni.
22
Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, naye mtu mwenye hasira ya haraka hutenda dhambi nyingi.
23
Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.
24
Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; huapishwa lakini hathubutu kushuhudia.
25
Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama.
26
Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana.
27
Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki.
Settings