Mika 5:2-5
2
“Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, kutoka milele.”
3
Kwa hiyo Israeli utaachwa mpaka wakati mwanamke aliye na utungu atakapozaa na ndugu zake wengine warudi kujiunga na Waisraeli.
4
Atasimama na kulichunga kundi lake katika nguvu ya Bwana, katika utukufu wa jina la Bwana Mungu wake. Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
5
Naye atakuwa amani yao. Wakati Mwashuru atakapovamia nchi yetu na kupita katika ngome zetu, tutawainua wachungaji saba dhidi yake, hata viongozi wanane wa watu.
Settings