Marko 15:1-5
1
Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato.
2
Pilato akamuuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.”
3
Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi.
4
Pilato akamuuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.”
5
Lakini Yesu hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa.
Settings