Marko 11:4-6
4
Wakaenda, wakamkuta mwana-punda amefungwa kando ya barabara, karibu na mlango wa nyumba.
5
Walipokuwa wanamfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakawauliza, “Mna maana gani mnapomfungua huyo mwana-punda?”
6
Wakawajibu kama vile Yesu alivyokuwa amewaagiza, nao wale watu wakawaruhusu.