Walawi 11:13-23
13
“ ‘Wafuatao ndio ndege watakaokuwa machukizo kwenu, hivyo msiwale kwa sababu ni chukizo: tai, furukombe, kipungu,
14
mwewe mwekundu, aina zote za mwewe mweusi,
15
aina zote za kunguru,
16
mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga, shakwe, aina zote za kipanga,
17
bundi, mnandi, bundi mkubwa,
18
mumbi, mwari, nderi,
19
korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.
20
“ ‘Wadudu wote warukao ambao hutembea kwa miguu minne watakuwa chukizo kwenu.
21
Lakini wako viumbe wenye mabawa ambao hutembea kwa miguu minne mtakaowala: wale wenye vifundo katika miguu yao ya kurukaruka juu ya ardhi.
22
Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi.
23
Lakini viumbe wengine wote wenye mabawa na wenye miguu minne ni machukizo kwenu.
Settings