Maombolezo 5:1-10
1
Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu.
2
Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zetu kwa wageni.
3
Tumekuwa yatima wasio na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.
4
Ni lazima tununue maji tunayokunywa, kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.
5
Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu, tumechoka na hakuna pumziko.
6
Tumejitolea kwa Misri na Ashuru tupate chakula cha kutosha.
7
Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena, na sisi tunachukua adhabu yao.
8
Watumwa wanatutawala na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.
9
Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya upanga jangwani.
10
Ngozi yetu ina joto kama tanuru, kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.
Settings