Yohana 8:31-36
31
Kisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli.
32
Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”
33
Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Abrahamu, nasi hatujawa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”
34
Yesu akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35
Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima.
36
Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.
Settings