Skip to content
Ayubu 4:12-17

Ayubu 4:12-17

12
“Neno lililetwa kwangu kwa siri, masikio yangu yakasikia mnongʼono wake.
13
Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku, hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu,
14
hofu na kutetemeka kulinishika na kufanya mifupa yangu yote itetemeke.
15
Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu, nazo nywele za mwili wangu zikasimama.
16
Yule roho akasimama, lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani. Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu, kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti:
17
‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu? Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options