Ayubu 36:24-33
24
Kumbuka kuzitukuza kazi zake, ambazo watu wamezisifu katika wimbo.
25
Wanadamu wote wameiona; watu wanaikazia macho kwa mbali.
26
Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27
“Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;
28
mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.
29
Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.
30
Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka, naye huvifunika vilindi vya bahari.
31
Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, na kuwapa chakula kwa wingi.
32
Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi, na kuuagiza kulenga shabaha yake.
33
Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja; hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.
Settings