Ayubu 3:13-18
13
Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani. Ningekuwa nimelala na kupumzika
14
pamoja na wafalme na washauri wa dunia, waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu,
15
pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu, waliozijaza nyumba zao kwa fedha.
16
Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu, kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga?
17
Huko waovu huacha kusumbua na huko waliochoka hupumzika.
18
Wafungwa nao hufurahia utulivu wao, hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa.
Settings