Skip to content
Ayubu 3:20-26

Ayubu 3:20-26

20
“Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni, na hao wenye uchungu kupewa uhai,
21
wale wanaotamani kifo ambacho hakiji, wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa,
22
ambao hujawa na furaha, na hushangilia wafikapo kaburini?
23
Kwa nini uhai hupewa mtu ambaye njia yake imefichika, ambaye Mungu amemzungushia boma?
24
Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula; kusononeka kwangu kunamwagika kama maji.
25
Lile nililokuwa naliogopa limenijia; lile nililokuwa ninalihofia limenipata.
26
Sina amani, wala utulivu; sina pumziko, bali taabu tu.”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options