Skip to content
Ayubu 3:1-11

Ayubu 3:1-11

1
Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.
2
Kisha akasema:
3
“Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali, nao usiku ule iliposemekana, ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’
4
Siku ile na iwe giza; Mungu juu na asiiangalie; nayo nuru isiiangazie.
5
Giza na kivuli kikuu kiikalie tena; wingu na likae juu yake; weusi na uifunike nuru yake.
6
Usiku ule na ushikwe na giza kuu; usihesabiwe katika siku za mwaka, wala usihesabiwe katika siku za mwezi wowote.
7
Usiku ule na uwe tasa; sauti ya furaha na isisikike ndani yake.
8
Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku, wale walio tayari kumwamsha Lewiathani.
9
Nyota zake za alfajiri na ziwe giza; nao ungojee mwanga bila mafanikio, wala usiuone mwonzi wa kwanza wa mapambazuko,
10
kwa sababu huo usiku haukunifungia mlango wa tumbo la mama yangu, ili kuyaficha macho yangu kutokana na taabu.
11
“Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa? Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni?
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options