Ayubu 28:1-11
1
“Kuna machimbo ya fedha, na mahali dhahabu isafishwapo.
2
Chuma hupatikana ardhini, nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini.
3
Mwanadamu hukomesha giza; huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini katika giza jeusi sana.
4
Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba.
5
Ardhi, ambako chakula hutoka, chini hugeuzwa kwa moto;
6
yakuti samawi hutoka katika miamba yake, nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu.
7
Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, wala hakuna jicho la mwewe lililoiona.
8
Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, wala simba azungukaye huko.
9
Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, na kuiacha wazi mizizi ya milima.
10
Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; macho yake huona hazina zake zote.
11
Hutafuta vyanzo vya mito na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.
Settings