Ayubu 20:22-29
22
Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; taabu itamjia kwa nguvu zote.
23
Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake.
24
Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, mshale wa shaba utamchoma.
25
Atauchomoa katika mgongo wake, ncha ingʼaayo kutoka ini lake. Vitisho vitakuja juu yake;
26
giza nene linavizia hazina zake. Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.
27
Mbingu zitaweka wazi hatia yake, nayo nchi itainuka kinyume chake.
28
Mafuriko yataichukua nyumba yake, maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.
29
Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu, urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”
Settings