Ayubu 13:20-28
20
“Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, nami sitajificha uso wako:
21
Ondoa mkono wako uwe mbali nami, nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.
22
Niite kwenye shauri nami nitajibu, au niache niseme, nawe upate kujibu.
23
Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.
24
Kwa nini kuuficha uso wako na kunihesabu mimi kuwa adui yako?
25
Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu?
26
Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.
27
Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. Unazichunga kwa makini njia zangu zote kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.
28
“Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, kama vazi lililoliwa na nondo.
Settings