Ayubu 11:7-12
7
“Je, waweza kujua siri za Mungu? Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi?
8
Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: wewe waweza kujua nini?
9
Kipimo chake ni kirefu kuliko dunia, nacho ni kipana kuliko bahari.
10
“Kama akija na kukufunga gerezani, na kuitisha mahakama, ni nani awezaye kumpinga?
11
Hakika anawatambua watu wadanganyifu; naye aonapo uovu, je, haangalii?
12
Mpumbavu aweza kuwa mwenye hekima, endapo mtoto wa punda-mwitu atazaliwa mwanadamu.
Settings