Skip to content
Yeremia 50:8-16

Yeremia 50:8-16

8
“Kimbieni kutoka Babeli; ondokeni katika nchi ya Wakaldayo tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi.
9
Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. Watashika nafasi zao dhidi yake, naye kutokea kaskazini atatekwa. Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari, ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.
10
Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara; wote wamtekao nyara watapata za kutosha,” asema Bwana.
11
“Kwa sababu hushangilia na kufurahi, wewe utekaye urithi wangu, kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka, na kulia kama farasi dume,
12
mama yako ataaibika mno, yeye aliyekuzaa atatahayari. Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote, atakuwa nyika, nchi kame na jangwa.
13
Kwa sababu ya hasira ya Bwana hatakaliwa na mtu, lakini ataachwa ukiwa kabisa. Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote.
14
“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wowote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana.
15
Piga kelele dhidi yake kila upande! Anajisalimisha, minara yake inaanguka, kuta zake zimebomoka. Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana, mlipizeni kisasi; mtendeeni kama alivyowatendea wengine.
16
Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja na akimbilie kwenye nchi yake mwenyewe.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options