Skip to content
Yeremia 46:2-12

Yeremia 46:2-12

2
Kuhusu Misri: Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Frati na Nebukadneza mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:
3
“Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo, mtoke kwa ajili ya vita!
4
Fungieni farasi lijamu, pandeni farasi! Shikeni nafasi zenu mkiwa mmevaa chapeo! Isugueni mikuki yenu, vaeni dirii vifuani!
5
Je, ninaona nini? Wametiwa hofu, wanarudi nyuma, askari wao wameshindwa. Wanakimbia kwa haraka pasipo kutazama nyuma, tena kuna hofu kuu kila upande,” asema Bwana.
6
Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia, wala wenye nguvu hawawezi kutoroka. Kaskazini, kando ya Mto Frati, wanajikwaa na kuanguka.
7
“Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili, kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi?
8
Misri hujiinua kama Mto Naili, kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi. Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia, nitaiangamiza miji na watu wake.’
9
Songeni mbele, enyi farasi! Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi, Endeleeni mbele, enyi mashujaa: watu wa Kushi na Putu wachukuao ngao, watu wa Ludi wavutao upinde.
10
Lakini ile siku ni ya Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, siku ya kulipiza kisasi, kisasi juu ya adui zake. Upanga utakula hata utakapotosheka, hadi utakapozima kiu yake kwa damu. Kwa maana Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati.
11
“Panda hadi Gileadi ukapate zeri, ee Bikira Binti wa Misri. Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio; huwezi kupona.
12
Mataifa yatasikia juu ya aibu yako, kilio chako kitaijaza dunia. Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine, nao wataanguka chini pamoja.”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options