Yeremia 25:17-26
17
Hivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwa Bwana, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa:
18
Yaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na maafisa wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kuchukiza, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo;
19
pia Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote,
20
pia wageni wote walioko huko; wafalme wote wa nchi ya Usi; wafalme wote wa Wafilisti (wale wa Ashkeloni, Gaza, Ekroni na watu walioachwa huko Ashdodi);
21
Edomu, Moabu na Amoni;
22
wafalme wote wa Tiro na Sidoni; wafalme wa nchi za pwani ngʼambo ya bahari;
23
Dedani, Tema, Buzi na wote walio maeneo ya mbali;
24
wafalme wote wa Arabuni na wafalme wote wa watu wageni wanaoishi katika jangwa;
25
wafalme wote wa Zimri, Elamu na Umedi;
26
na wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki atakunywa pia.
Settings