Skip to content
Isaya 24:1-12

Isaya 24:1-12

1
Tazama, Bwana ataifanya dunia kuwa ukiwa na kuiharibu, naye atauharibu uso wake na kutawanya wakaao ndani yake:
2
ndivyo itakavyokuwa kwa makuhani na kwa watu, kwa bwana na kwa mtumishi, kwa bibi na kwa mtumishi wake wa kike, kwa muuzaji na kwa mnunuzi, kwa mkopaji na kwa mkopeshaji, kwa mdaiwa na kwa mdai.
3
Dunia itaharibiwa kabisa na kutekwa nyara kabisa. Bwana amesema neno hili.
4
Dunia inakauka na kunyauka, dunia inanyongʼonyea na kunyauka, waliotukuzwa wa dunia wananyongʼonyea.
5
Dunia imetiwa unajisi na watu wake; wameacha kutii sheria, wamevunja amri na kuvunja agano la milele.
6
Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia, watu wake lazima waichukue hatia yao. Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa, nao waliosalia ni wachache sana.
7
Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka, watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni.
8
Furaha ya matoazi imekoma, kelele za wenye furaha zimekoma, shangwe za kinubi zimenyamaza.
9
Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo, kileo ni kichungu kwa wanywaji wake.
10
Mji ulioharibiwa umekuwa ukiwa, mlango wa kila nyumba umefungwa.
11
Barabarani wanalilia kupata mvinyo, furaha yote imegeuka kuwa majonzi, furaha yote imefukuziwa mbali na dunia.
12
Mji umeachwa katika uharibifu, lango lake limevunjwa vipande.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options