Skip to content
Waefeso 5:23-27

Waefeso 5:23-27

23
Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa, ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake.
24
Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.
25
Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake
26
kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake,
27
apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na lisilo na hatia.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options