1
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema.
2
“Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi,
3
“upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”
4
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.