Danieli 5:25-31
25
“Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa: mene, mene, tekeli na peresi
26
“Hii ndiyo maana ya maneno haya: “Mene: Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha.
27
Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.
28
Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”
29
Ndipo kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu katika ufalme.
30
Usiku ule ule, Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa,
31
naye Dario Mmedi akashika ufalme akiwa na miaka sitini na miwili.
Settings