Skip to content
1 Samweli 21:10-15

1 Samweli 21:10-15

10
Siku ile Daudi akamkimbia Sauli na kwenda kwa Akishi mfalme wa Gathi.
11
Lakini watumishi wa Akishi wakamwambia, “Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema: “ ‘Sauli amewaua elfu zake, naye Daudi makumi elfu yake’?”
12
Daudi akayaweka maneno haya moyoni naye akamwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi.
13
Basi akajifanya mwendawazimu mbele yao; naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango na kuachia udelele kutiririka kwenye ndevu zake.
14
Akishi akawaambia watumishi wake, “Tazameni mtu huyu! Ana wazimu! Kwa nini mnamleta kwangu?
15
Je, mimi nimepungukiwa na wenda wazimu kiasi kwamba mmeniletea mtu huyo hapa aendelee kufanya hivi mbele yangu? Je, ilikuwa ni lazima mtu huyo aje nyumbani kwangu?”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options