Rukia maudhui

Zaburi75

Shukrani kwa Mungu Aliye Karibu

1
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo. Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu.

Mungu Atangaza Hukumu Yake ya Haki

2
Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki.
3
Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

Onyo Dhidi ya Majivuno ya Kujisifu

4
Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.
5
Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”
6
Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.
7
Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine.
8
Mkononi mwa Bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho.

Ushindi wa Wenye Haki

9
Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.
10
Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.
Use arrow keys to navigate
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options