Skip to content

Zaburi 13

Kilio cha Kuachwa 1–2

1
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Mpaka lini, Ee Bwana? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako mpaka lini?
2
Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda mpaka lini?

Ombi la Mungu Kuingilia 3–4

3
Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.
4
Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

Kugeukia Tumaini na Sifa 5–6

5
Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.
6
Nitamwimbia Bwana, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Maandiko ya Biblia: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)™, © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. · CC BY-SA 4.0“Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc., used with permission.