Zaburi123
Listen to this chapter
0:00
0:00
1
Wimbo wa kwenda juu. Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni.
2
Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mtumishi wa kike yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu, mpaka atakapotuhurumia.
3
Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu, kwa maana tumevumilia dharau nyingi.
4
Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.
Use ← → arrow keys to navigate
Settings
Reading Style
Typeface
Font Size px
Options
Study Note