Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Reverence: For the aged

5 mistari · 2 vipengele

Mistari kuhusu For the aged

  1. “ ‘Uwapo mbele ya mzee, simama ili kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

  2. Basi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye.

  3. Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka.

  4. Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema: “Mimi ni mdogo kwa umri, nanyi ni wazee; ndiyo sababu niliogopa, sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua.

  5. Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’