Skip to content
Warumi 12:17-21

Warumi 12:17-21

17
Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote.
18
Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote.
19
Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana.
20
Badala yake: “Kama adui yako ana njaa, mlishe; kama ana kiu, mpe kinywaji. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”
21
Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options