Skip to content
Warumi 10:9-13

Warumi 10:9-13

9
Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.
10
Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu.
11
Kama yasemavyo Maandiko, “Yeyote amwaminiye hataaibika kamwe.”
12
Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao.
13
Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa.”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options