Zaburi 87:2-6
2
Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.
3
Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:
4
“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”
5
Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”
6
Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”
Settings