Skip to content
Zaburi 68:7-18

Zaburi 68:7-18

7
Ee Mungu, ulipowatangulia watu wako, ulipopita nyikani,
8
dunia ilitikisika, mbingu zikanyesha mvua, mbele za Mungu, Yule wa Sinai, mbele za Mungu, Mungu wa Israeli.
9
Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka.
10
Ee Mungu, watu wako waliishi huko, nawe kwa wingi wa utajiri wako uliwapa maskini mahitaji yao.
11
Bwana alitangaza neno, waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa:
12
“Wafalme na majeshi walikimbia upesi, watu waliobaki kambini waligawana nyara.
13
Hata ulalapo katikati ya mioto ya kambini, mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha, manyoya yake kwa dhahabu ingʼaayo.”
14
Wakati Mwenyezi alipowatawanya wafalme katika nchi, ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Salmoni.
15
Milima ya Bashani ni milima iliyotukuka, milima ya Bashani ina vilele vilivyochongoka.
16
Enyi milima yenye vilele vilivyochongoka, kwa nini mnakazia macho kwa wivu, katika mlima Mungu anaochagua kutawala, ambako Bwana mwenyewe ataishi milele?
17
Magari ya Mungu ni makumi ya maelfu, na maelfu ya maelfu; Bwana amekuja kutoka Sinai hadi katika patakatifu pake.
18
Ulipopanda juu, uliteka mateka, ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu, hata kutoka kwa wale walioasi, ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options