Skip to content
Zaburi 40:8

Zaburi 40:8

Inaonyesha mstari 8 pamoja na muktadha unaouzunguka.
5
Ee Bwana Mungu wangu, umefanya mambo mengi ya ajabu. Mambo uliyopanga kwa ajili yetu hakuna awezaye kukuhesabia; kama ningesema na kuyaelezea, yangekuwa mengi mno kuyaelezea.
6
Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu; sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji.
7
Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kunihusu katika kitabu.
8
Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”
9
Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee Bwana, kama ujuavyo.
10
Sikuficha haki yako moyoni mwangu; ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha upendo wako na kweli yako mbele ya kusanyiko kubwa.
11
Ee Bwana, usizuilie huruma zako, upendo wako na kweli yako daima vinilinde.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 90 chars

Options